Maisha jambo muhimu, mejaliwa na Jalali
Binadamu tujikimu, tupate kufika mbali
Tufanye hilo jukumu, sirudiye ya awali
Maisha jambo muhimu,banadamu usichoke

Kama wewe ni tabibu, wafanya zahanitini
Dadako ataka jibu, yamkumba Maishani
Sijitose kwa taabu, weewe Ndiye rubani
Maisha jambo muhimu,banadamu usichoke

Maisha mema zawadi, maisha bila karaha
Wakongwe wetu wa jadi, lishinda kwa zao raha
Huyo ni wako hasidi?, mtunze yeye kwa staha
Maisha jambo muhimu,banadamu usichoke

Sisahau tumaini, nguzo kuu ya maisha
Umelegea kwa nini?, tumaini limekwisha!
Hilo sikukate ini, maadamu litakwisha
Maisha jambo muhimu,banadamu usichoke

Tuyaishi ya dhamani ,tuishi bila kuchoka
Kuongezea imani, tutashinda kwa Hakika
Kakako yule kimani, hataki kutikisika
Maisha jambo muhimu,banadamu usichoke

Uvivu tuiepuke, chunga isikukamate
Ujinga usitufike, kamwe sitemewe mate
Milele sitikisike, na tusimame kidete
Maisha jambo muhimu,banadamu usichoke

Shabaha lile lilenge, ufaulu masomoni
Utanywa maji maenge, kifaulu namba wani
Maisha mema yatunge, maisha siyo na utani
Maisha jambo muhimu,banadamu usichoke

Kuishi Kuna dhamani, tumepewa na Rabuka
Kuchoka hivo kwa nini, kweli mi mi ninamaka
Wateseka Maishani, raha ndio unataka
Maisha jambo muhimu,banadamu usichoke

Na kitanzi Sijaribu, na maovu jiepushe
Wewe huoni aibu, kwenye kamba ujishushe
Usipatwe na taabu Usipatwe na kasheshe
Maisha jambo muhimu,banadamu usichoke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *