Machozi yatiririka, kimwona nimpendaye
Moyo wangu wakatika, kimwona nimjuaye
Mtima wangu wataka kukaa pamoja naye
Moyo wangu wakupenda, kweli wewe wanipenda?
Imetimia awamu, nipasue waziwazi
Mtima wavuja damu, kamwe mi sio bazazi
Kuwa wako Nina hamu, na mapenzi yawe wazi
Moyo wangu wakupenda,kweli wewe wanipenda?
Wajua nitakumisi, lakini nitakupata
Kwa mapenzi mi sio fisi, Mtima wangu wapapa
Mwili wako ni fususi, nasema papa kwa hapa
Moyo wangu wakupenda,kweli wewe wanipenda?
Ulitaka kunambiya, we bado hujawadiya
Nami nikakuambiya, mi nakupenda piya
Sijaribu kukimbia, Kwani mi nitajliya
Moyo wangu wakupenda,kweli wewe wanipenda?
Ukingoni nimefika, kutakia siha njema
Tena upate fanaka, Tena ujaliwe mema
Kwako sasa nimefika, kwangu siwe na shutuma
Moyo wangu wakupenda,kweli wewe wanipenda?

2 Comments

 1. elvis

  March 9, 2018 at 7:38 am

  its damn hot……

  Reply
 2. weltonkoech

  March 9, 2018 at 8:17 am

  that’s nice work endelea ivo ivo utakuwa bingwa

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *